Kendrick Lamar, Davido Walivyotisha Tuzo za BET 2018
JUZI usiku (Jumapili), ndani ya jengo la burudani la L.A Live, lililotulia pale kwenye Mtaa wa South Park, Downtown, Los Angeles nchini Marekani, kituo maarufu cha televisheni kiitwacho Black Entertainment kilikuwa kinagawa tuzo zake za BET.
Tuzo hizi ambazo zilikuwa zinatolewa kwa mara ya 19 mfululizo, ni mahususi kwa ajili ya tasnia ya muziki ingawa zinapapasa kwa kiasi kidogo kwenye aina nyingine za burudani ikiwemo muvi, Madj na waandaaji wa muziki.
Tuzo za mwaka huu zilikuwa ni za kibabe. Ukiachana na mastaa mbalimbali waliolala usingizi mnono pembeni yao wakiwa wamevuna tuzo za heshima kwenye kazi zao, mengi mazuri yalitokea mbele ya ‘host’ Jamie Foxx.
Risasi Vibes, linakumegea baadhi ya matukio yaliyopendezesha usiku huo pamoja na washindi wa tuzo zenyewe!
ALIYEFUNGUA NI HUYU HAPA
Johnny Reed McKenzie, Jr. anafahamika zaidi kwa wapenzi wa muziki duniani kwa jina la Jay Rock. Mshikaji huyo ambaye amezaliwa na kukulia Watts, California, ndiye aliyefungua usiku wa BET, kwa shoo kali kwa ‘kupafomu’ wimbo wake mpya uitwao Win.
Kitendo hicho kilionekana ‘kuwasapraiz’ mashabiki kwani mawazo ya wengi hata komenti kwenye mitandao ya kijamii walifikiri Jay, angepafomu wimbo wake unaopendwa na mashabiki uitwao King’s Dead ambao amewashirikisha Kendrick Lamar, Future na James Blake, ambao pia umetumika kama ‘soundtrack’ kwenye Filamu ya Black Panther. Pamoja na hilo, bado alipokea shangwe za kutosha!
MEEK MILL AMUENZI XXXTENTACION
Rapa Meek Mill, pia alipata nafasi ya kufanya shoo kwenye usiku huo wa BET, ambapo alipafomu wimbo wake mpya uitwao Stay Woke. Meek, alipanda jukwaani kufanya yake alikuwa ametupia tisheti yenye picha ya Rapa XXXTentacion, aliyeuawa kwa kupigwa risasi huko Florida, Marekani.
SNOOP DOGG NAYE AWAPELEKA WATU KANISANI
Burudani ilikuwa ni ya aina yake, ndiyo maana huwezi kuacha kuziita tuzo hizi kwamba ni za Kibabe. Mkongwe ambaye ni ‘legendary’ kwenye Gemu la Muziki wa Hip Hop duniani, naye alifanya makamuzi ya kibabe pale alipopanda jukwaani kutoa burudani kwenye usiku huo.
Snoop alianza kwa kutwanga ngoma zake kali za mwaka 1990. Alianza na Who Am I? (What’s My Name?), baadaye akagonga wimbo alioutoa miaka ya 2000 uitwao The Next Episode.
Baada ya hapo Snoop aliwapeleka watu kanisani. Unajua alifanya nini? Alicheza nyimbo kadhaa kutoka kwenye albamu yake ya 16, iitwayo Bible of Love aliyoitoa Machi 16, mwaka huu.
HAWA NAO WALI-KAMUA HA-TARI!
Wana-muziki wengine ambao walipata nafasi na kufanya makamuzi ya maana ni YG, Nick Minaj, Childish Gambino, aliyekamua Wimbo wa This is America. Wengine ni Chris Brown, SZA, Teyena Taylor na Ella Mai.
UGA-WAJI WA TUZO ULI-KUWA HIVI!
Wengi walifikiri kwenye Tuzo za BET za Mwaka huu, Dj Khaled angetisha kwani alikuwa amechaguliwa kwenye vipengele sita, akishindania tuzo tofautitofauti.
Lakini haikuwa hivyo, aliambulia tuzo moja tu huku Kendrick Lamar akipata mbili na kwa upande wa Afrika, Davido ndiye aliyetisha kwa kuipeperusha vyema bendera ya Nigeria baada ya kuvuna pia tuzo moja. Vipengele vilikuwa hivi;
MWANAMUZIKI BORA WA KIKE WA R&B/ POP
Mshindi: Beyonce
MWANAMUZIKI BORA WA KIUME WA R&B / POP
Mshindi: Bruno Mars
KUNDI BORA
Mshindi: Migos
KOLABO BORA
Iliyoshinda: DJ Khaled feat. Rihanna & Bryson Tiller – Wild Thoughts
MWANAMUZIKI BORA WA KIUME WA HIP HOP
Mshindi: Kendrick Lamar
MWANAMUZIKI BORA WA KIKE WA R&B/ POP
Mshindi: Beyonce
MWANAMUZIKI BORA WA KIUME WA R&B / POP
Mshindi: Bruno Mars
KUNDI BORA
Mshindi: Migos
KOLABO BORA
Iliyoshinda: DJ Khaled feat. Rihanna & Bryson Tiller – Wild Thoughts
MWANAMUZIKI BORA WA KIUME WA HIP HOP
Mshindi: Kendrick Lamar
MWANAMUZIKI BORA WA KIKE WA HIP HOP
Mshindi: Cardi B
VIDEO BORA YA MWAKA
Mshindi: Drake – God’s Plan
DAIREKTA BORA WA VIDEO
Mshindi: Ava Duvernay
MWANAMUZIKI BORA ANAYECHIPUKIA
Mshindi: SZA
WIMBO BORA WA GOSPO / KUHAMASISHA
Mshindi: Lecrae feat. Tori Kelly – I’ll Find You
MSANII BORA NJE YA MAREKANI
Mshindi: Davido (Nigeria)
MUIGIZAJI BORA WA KIKE
Mshindi: Tiffany Haddish
MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Mshindi: Chadwick Boseman
FILAMU BORA YA MWAKA
Iliyoshinda; Black Panther
MWANAMICHEZO BORA WA KIKE
Mshindi: Serena Williams
MWANAMICHEZO BORA WA KIUME
Mshindi: LeBron James
ALBAMU BORA YA MWAKA
Mshindi: DAMN – Kendrick Lamar
CHAGUO LA Coca-Cola
Mshindi: Cardi B – Bodak Yellow
Boniphace Ngumije
Comments are closed.