The House of Favourite Newspapers

Kenya: Odinga Aendelea Kudai yeye Ndiye Mshindi halali wa Uchaguzi wa rais wa Agosti mwaka jana

0
Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga

Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumatatu alisisitiza kuwa yeye ndiye mshindi halali wa uchaguzi wa mwaka jana, na kuzidisha madai ya udangayifu miezi mitano baada ya uchaguzi.

Odinga alishindwa kwa idadi ndogo ya kura na William Ruto, kulingana na matokeo rasmi, licha ya kuungwa mkono na chama kilichokuwa madarakani.

“Tuna uhakika, bila shaka, kwamba ushindi wetu uliibiwa,” mkongwe huyo wa kisiasa mwenye umri wa miaka 78 aliuambia mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya watu mashariki mwa mji mkuu Nairobi.

Akitaja takwimu kutoka kwa mtoa taarifa za siri ndani ya tume huru ya uchaguzi na mipaka(IEBC) iliyosimamia uchaguzi huo, Odinga alidai alishinda kwa zaidi ya kura milioni mbili.

Baada ya matokeo kutangazwa, alidai kulikuwa na udanganyifu na udukuzi wa seva za tume ya uchaguzi na kupinga matokeo katika kesi ambayo haikufaulu iliyowasilishwa kwenye mahakama ya juu ya Kenya.

MIKUTANO ya HADHARA, FAIDA na HASARA ZAKE – “MPIRA UPO UWANJANI MWAMUZI ni DAKIKA 90”

Leave A Reply