The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Akina Halima Mdee, Jaji Atoa Uamuzi Sasa Kuanza Kuhojiwa Mahakani

0

LEO ikiwa ni Septemba 2, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga Septemba 30, mwaka huu kuanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na wabunge wa viti Maalum (CHADEMA),akiwemo  Halima Mdee na wenzake 18.

 

Mahakama hiyo pia imeridhia ombi la kuitwa mahakamani Mbuge Grace Tendega na Hawa Mwifunga wafike tarehe hiyo ili wahojiwe na mawakili wa wajibu maombi wa kwanza ambao ni CHADEMA. Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji wa mahakama hiyo Cyprian Mkeha, baada ya pande zote mbili katika kesi hiyo kuondoa mapingamizi yao ya awali

 

Kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa ombi la mawakili wa Mdee na wenzake la kutaka kuwasilisha mapingamizi ya awali ambapo mahakama iliwakubalia ombi hilo.

Mdee na wenzake 18 walifungua kesi hiyo Julai 21 mwaka huu mahakamani hapo dhidi ya Chadema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakipinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema kuwavua uanachama, Mei 11, mwaka 2022.

Leave A Reply