The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Bodi ya Wadhamini Cuf Kuanza Kusikilizwa (Picha&Video)

bodi-ya-baraza-la-wadhamini-la-cuf-1

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Maharagande Mbarala (kushoto) akizungumza na wanahabari baada ya kutoka katika chumba cha Mahakama Kuu, Dar es Salaam.

bodi-ya-baraza-la-wadhamini-la-cuf-2 bodi-ya-baraza-la-wadhamini-la-cuf-3

Wanachama wa CUF wakitoka lango kuu la mahakama hiyo leo.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam itaanza kusikiliza hivi karibuni kesi ya Bodi ya Baraza la Wadhamini la CUF dhidi ya Jaji Francis Mutungi baada ya kuisajili na kuipatia namba ya usajili 23 ya mwaka 2016.

Akizungumza na wanahabari baada ya kutoka katika chumba cha mahakama leo, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Maharagande Mbarala, amesema kuwa kesi hiyo ilikuwa ikipangiwa majaji wa kuisikiliza.
Katika maombi hayo namba 75 ya mwaka 2016 walalamikiwa wengine ni Prof. Lipumba na wanachama 12 wa chama hicho waliosimamishwa.

Tazama video kamili hapa;

Bodi hiyo ya wadhamini ilifungua maombi hayo wiki kadhaa zilizopita wakili wao akiwa ni Juma Nassoro wakiiomba mahakama itengue na kupitia uamuzi wa barua ya Jaji Mutungi kumtambua Lipumba kuwa mwenyekiti.

Wakili Nassoro wiki iliyopita alisema kuwa mahakama ilikubali maombi hayo yaliyofunguliwa ya kuomba ifute barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, inayomtambua Prof. Lipumba kuwa ndiye mwenyekiti wa CUF.

Alisema pia mahakama ilikubaliana na zuio lao dhidi ya msajili kufanya kazi zake nje ya utaratibu ambao amepewa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.