The House of Favourite Newspapers

Yaliyojiri Kesi ya Bosi wa Jamii Media Mahakamani Kisutu Leo

0

melo-1Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media (wa pili kulia), akiwa na watu wake wa karibu aliyoambatana nao mahakamani hapo.

DAR ES SALAAM: Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Melo, iliyokuwa isikilizwe leo Januari 16, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirishwa hadi Februari 16, 2017 kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

melo-2

Akitoa uamuzi huo baada ya Wakili wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na haujakamilika bado, hivyo Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu, Victoria Nongwa, aliutaka upande wa Jamhuri kukamilisha haraka upelelezi wa kesi hiyo ili iweze kusikilizwa kabla ya kuiahirisha na kuipanga tarehe tajwa hapo juu.

melo-3

Maxence Melo anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply