The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Idris Yakwama Kortini

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi inayomkabili Idriss Sultani, Msanii wa Vichekesho na mwenzake Innocent Maiga baada ya upande wa serikali kushindwa kukamilisha kuandaa hoja za awali.

 

Tarehe 27 Mei 2020 kesi hiyo iliahirishwa hadi leo tarehe 9 Juni 2020 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali, lakini upande wa serikali umeeleza mahakama, haujamaliza kuandaa hoja za awali na kuahirishwa hadi tarehe 9 Julai 2020 kwa ajili ya kusoma hoja hizo.

 

Idriss na Maiga walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo tarehe 27 Mei 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Rashid Chaungu.
Idriss anashitakiwa kwa kutumia laini ya simu ambayo ina umiliki wa mtu mwingine wa Maiga, naye Maiga anakabiliwa na kosa la kumruhusu mtu mwingine (Idriss) kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake.

 

Wakati akisoma mashitaka hayo, Wankyo Simom wakili wa serikali mwandamizi akisaidiana na mawakili wa serikali Batlida Mushi na Estazia Wilson, alidai washtakiwa walitenda makosa hayo katika nyakati tofauti kati ya Desemba Mosi mwaka jana na tarehe 19 Mei 2020 katika eneo la Mbezi Beach ndani ya Wilaya ya Kinondoni.

 

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo na waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana na kutakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho na kusaini bondi ya Shilingi 15 milioni kila mmoja.

 

Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Jebra Kambole baada ya wakili Benedict Ishabakaki kuondolewa kuwakilisha washtakiwa kwa sababu atatumika kama shahidi wa upande wa Jamhuri kwa sababu alishuhudia washitakiwa akichukuliwa maelezo ya onyo Polisi.

 

Wakili Wankyo amedai wakili Ishabakaki hawezi kuendelea na uwakilishi huku pia akiwa ni shahidi wa Jamuhuri tunaomba asiwe kuruhusiwa kuendelea na uwakilishi.

Leave A Reply