The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Mke wa Bilionea Msuya Yaendelea Kisutu

msuya-2DAR ES SALAAM: Wakati sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya zikiwa zimemalizika, leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha tena uamuzi wa maombi ya mke wa aliyekuwa bilionea jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, aitwaye Miriam Msuya ya kufutiwa mashitaka ya madai ya mauaji ya wifi yake, Anethe Msuya,  yaliyotokea Mei 25, mwaka jana, Kigamboni Dar.

msuya-1Uamuzi huo ungetolewa leo lakini kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 9, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Magreth Bankika, aliyesema kesi ilitajwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi leo lakini kwa kuwa wakili wa utetezi Peter Kibatala hakuwepo mahakamani, ikabidi apange siku nyingine ya uamuzi. Cap: Miriam Msuya alipofikishwa mahakamani Kisutu leo.

Comments are closed.