The House of Favourite Newspapers

KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU YAKWAMA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na mwenzake  kwa madai yakuwa  shahidi wa upande wa mashtaka ana dharura.

 

Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru Vitalis Peter amedai leo Novemba 13, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika Kesi hiyo amepatwa na dharura.

 

Kutokana na hiyo, Hakimu Simba alisema kwa mtindo huo kesi hiyo haitomalizika kwa wakati, na akashauri mawakili kuwa wanaleta mashahidi wawili Wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea na kutoa ushahidi wake.

 

Upande wa utetezi uliwakikishwa na Wakili Alex Mgongolwa ambaye aliwataka mashahidi wanaokwenda kutoa ushahidi katika Kesi hiyo wajulikane na kwamba upande wa mashtaka unapoona shahidi wanayemtafuta anahitilafu watafute mwingine.

 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 27 na 28, mwaka huu ambapo itaedelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

 

 

Katika kesi hiyo, Gugai na wenzake, George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato chake halali.

Comments are closed.