The House of Favourite Newspapers

Ishu ya Diamond na Rayvanny…. Mwana FA Akinzana na BASATA

Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Hamis Mwinjuma aka ‘Mwana FA’, ameomba adhabu waliyopewa wanamuziki Rayvanny na Diamond Platnumz kuhusiana na wimbo wao wa ‘Mwanza’ ipunguzwe  au ifutwe ili “kutowaumiza” wasanii hao.

 

Mwana FA ametoa wito huo leo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea ofisi za Basata ambapo alisema: “Nimeona nije kuongea na Baraza la Sanaa katika namna ambavyo naweza kuomba kama msanii, adhabu aidha ipunguzwe au iondolewe kwa kiwango kinachowezekana ili kufanya wasanii wasiumie.”

 

Alisema jukumu la kufungia wimbo si lake na yeye alichofanya ni kwenda kujaribu kuongea na kuwaomba watendaji kwamba adhabu watakayoichukua isiwaumize moja kwa moja wasanii hao hata kama kuna makosa yamefanyika.

 

“Uongozi mzima wa Wasafi Classic Baby (WCB) na wasanii wao wanapaswa kuandika barua ya kuomba radhi na kuomba kupunguziwa adhabu, halafu hao kama watendaji ndiyo wataamua la kufanya lakini la msingi naamini adhabu haitabaki kama ilivyotolewa siku ya jana,”alisisitiza.

 

ISIKUPITE: Barua Ya Wazi Ya Diamond Platnumz Kwenda Basata

Comments are closed.