The House of Favourite Newspapers

Khadija Kopa Adhihirisha Ukongwe Shoo ya Zuchu Dar Live

0

MALKIA wa Taarab Bongo, Khadija Omary Kopa usiku wa kuamkia leo jumamosi, mei 15, 2021 alidhihirisha umalkia na ukongwe wake wa muziki huo wakati akipiga shoo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live alipokuwa akimsindikiza mwanae Zuchu kutoka lebo ya WCB.

Katika shoo hiyo Khadija ndiye aliyeanza kupanda jukwaani na kugonga ngoma zake kali zisizochosha mashabiki ambapo ukumbini hapo palikuwa hapatoshi jinsi wapenzi wa taarabu walikuwa wakijimwaya kwa raha zao.

 

Miongoni mwa ngoma zilizoowadatisha mashabiki ni Mjini Chuo Kikuu ambayo mkongwe huyo alikuwa akiichagiza na mashairi ya papo hapo na kuwadatisha mashabiki waliofurika kiwanja hicho.

 

Kwa uhondo zaidi angalia picha.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

‘SHANGWE la EID’ – ZUCHU, JUMA NATURE, KHADIJA KOPA WANAWASHA MOTO JUKWAANI..

Leave A Reply