The House of Favourite Newspapers

Khalid Chokoraa Azuru Global

0

1    Mwanamuziki wa muziki wa Dansi Bongo Khalidi Chuma ‘Chokoraa’, akishuka kwenye gari lake tayari kwa kuingia ndani ya ofisi za Global Publishers LTD, kufanya ziara yake.

2Chokoraa akiwa kwenye chumba cha mapokezi akiomba maelekezo kutoka kwa dada wa mapokezi.

3Mhariri wa gazeti la Risasi Jumamosi Erick Evarist (kulia), akimfanyia mahojiano.

4Mhariri wa gazeti la Risasi Mchanganyiko Ojuku Abraham (kushoto), akizungumza machache na Chokoraa baada ya kutambulishwa kwake.

5Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa Oscar Ndauka (kushoto), akimkaribisha Chokoraa kwaajiri ya mazungumzo mafupi kwenye dawati lake.

6Mhariri wa gazeti la Ijumaa Amrani Kaima (kushoto), akimuonyesha baadhi ya kurasa za burudani Chokoraa.

7Mhariri wa gazeti la Uwazi Elvin Stambuli (kulia), akiongea jambo la Chokoraa baada ya utambulisho wake.

8Baadhi ya waandishi wa gazeti la Championi, Omari Mdose (kushoto) na Saidi Ally wakiwa katika pozi na Chokoraa.

9Mkuu wa kitengo ya IT Cralence Mlissa (kushoto), akisalimiana na Chokoraa baada ya kutambulishwa.

10Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi Saleh Ally (kulia), akifurahia jambo na Chokoraa baada ya kukutana nje ya ofisi wakati WA KUONDOKA KWAKE.

MWANAMUZIKI wa Muziki wa Dansi Tanzania, Khalid Chokara, leo amefanya ziara katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar.

Chokoraa ambaye hivi karibuni alirudi kwenye bendi yake ya zamani ya Africans Stars ‘Twanga Pepeta’, Jumamosi ya wikiendi hii anatarajiwa kutambulishwa rasmi urejeo wake katika shoo itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar.

Chokoraa ambaye licha ya kuwa ni mwanamuzi, lakini pia ni bondia wa ngumi za kulipwa nchini, amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na wafanyakazi wa Global katika shughului zao za kila siku ikiwemo uandaaji na uchapishaji wa magazeti yake ya Championi, Risasi, Ijumaa, Uwazi na  Amani.

Ikumbukwe kuwa, Chokoraa alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliokuwa wanaunda Bendi ya Mapacha Watatu pamoja na Jose Mara na Chaz Baba ambapo kabla ya kujiunga na bendi hiyo, alikuwa Twanga Pepeta na sasa amerejea nyumbani.

HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL.

Leave A Reply