The House of Favourite Newspapers

Khalid Chokoraa kutambulishwa rasmi Twanga, Juni 4

0

chokoraa-copySTAA wa Muziki wa Dansi aliyekuwa akiunda Kundi la Mapacha Watatu, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ amejivua rasmi umiliki wa bendi hiyo na kurejea bendi yake ya zamani, African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa Twanga, Asha Baraka alithibitisha kumpokea Chokoraa aliyewahi kutamba na Wimbo wa Kuachwa nk.

“Chokoraa rasmi Twanga na kwa mara ya kwanza ataanza kuonekana katika majukwaa akiwa na Twanga Juni 4, mwaka huu katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo ataungana na Chocky, Luiza katika uzinduzi wa albamu mpya ya 13 ya Usiyaogope Maisha,” alisema Asha.

Bendi ya Mapacha Watatu ilianzishwa Novemba 15, 2009 ikiwa na waimbaji waasisi, Jose Mara akitokea Bendi ya FM Academia, Khalid Chokoraa na Kalala Junior.

Leave A Reply