The House of Favourite Newspapers

Kiba, Vanessa wampotezea DiCaprio

0

Leonardo-DiCaprioLeonardo DiCaprio

Huku ikiwa imepita miaka 23 tangu staa wa Filamu ya Titanic, Leonardo DiCaprio kuanza kuitafuta Tuzo ya Oscar, hatimaye mwanzoni mwa wiki hii alifanikiwa kuipata lakini kitu kinachowashangaza wadau wengi ni kitendo cha wanamuziki Ali Kiba na Vanessa Mdee kumpotezea mshikaji kwa kutoposti picha zake mitandaoni.

King-KibaAli Kiba

Wadau wengi walijua kwamba wasanii hao wangeitumia nafasi hiyo kuweka picha za jamaa katika mitandao ili kuwafahamisha watu kwamba mbali na Jackie Chan, Lupita Nyong’o, pia katika Taasisi ya Wildlife wapo na staa huyo, kitu ambacho kingewafanya kuonekana kupata bahati kuwekwa na mastaa wakubwa duniani.

mdeea-778x1024Vanessa Mdee

“Washikaji hawajafanya poa, hii ndiyo ilikuwa nafasi ya kuwaoneshea Watanzania kwamba katika ishu ya Wildlife wapo pia na DiCaprio. Sasa wanataka nafasi zipi tena?” alihoji mmoja wa wadau aliyeongea na mwandishi wetu.

Leave A Reply