The House of Favourite Newspapers

Kibadeni Amaliza Vita ya Ubingwa Simba, Yanga

Kikosi cha Simba.

KOCHA na mche­zaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni’, amefunguka kuwa kama Simba itaendelea na moto ilionao, basi ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, tofauti na wapinzani wao Yanga ambao wa­naonekana kuchoka.

 

Simba inaongoza ligi kwa pointi 42, ikiwa ni tofauti ya pointi tano dhidi ya Yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 37 wakati Azam wakiwa nafasi ya tatu na pointi 35 hali inayosababisha ushindani kuwa mkubwa.

 

Kibadeni ameyasema hayo kufuatia kasi ya Simba msimu huu ambapo imefani­kiwa kushinda mechi 12 katika michezo 18 iliyocheza, wakitoka sare mechi sita huku wakiwa hawajapoteza mch­ezo wowote tofauti na Yanga ambao wamefan­ikiwa kushinda mechi kumi katika michezo 18 na wametoka sare michezo saba huku wak­ipoteza mmoja.

Yanga wakipiga mazoezi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kibadeni alisema kuwa Simba ya sasa ina nafasi kubwa ya kuweza kutwaa ubingwa iwapo wataendelea kukomaa na kasi waliyonayo hivi sasa katika Ligi Kuu Bara tofauti na wapinzani wao.

 

“Ligi ya msimu huu imekuwa ngumu na ushindani mkubwa kwa timu zote lakini kwa hizi timu za juu yaani Simba na Yanga kila moja inaonekana inapambana vilivyo, ila binafsi naona Simba wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuweza kutwaa ubingwa tofauti na Yanga.

 

“Lakini haitakuwa rahisi kama hawataweza kuendelea na kasi am­bayo wanayo hivi sasa, kwa sababu ukiangalia wameweza kushinda michezo mingi kwa mabao ya kuto­sha na ukiwaangalia Yanga wa sa­fari hii ni wazi hawapo vizuri kama tulivyozoea,” alisema Kibadeni.

 

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.