The House of Favourite Newspapers

Kibarua cha Sarri matatani, Arsenal yatinga ‘top 4’

KOCHA Maurizio Sarri sasa yupo katika wakati mgumu kutokana na kupambania kibarua chake, hiyo ni baada ya kushuhudia kikosi chake cha Chelsea kikiambulia kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Bournemouth, usiku wa kuamkia jana.

 

Kwa matokeo hayo sasa Chelsea imeshuka katika nafasi kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ kutoka nafasi ya nne hasi ya tano huku Arsenal ambayo haikuwa uwanjani ikipanda hadi nafasi ya nne.

 

Chelsea na Arsenal zote zina pointi 47 lakini Arsenal ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

 

Sarri aliajiriwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Napoli kuchukua nafasi ya Antonio Conte ambaye alifukuzwa kazi.

 

Licha ya kumtumia straika wake mpya, Gonzalo Higuain ambaye alishindwa kung’ara, bado matokeo hayo yameongeza presha kubwa kwake na sasa yupo hatarini kufukuzwa kutokana na rekodi ya klabu hiyo kutokuwa na uvumilivu wa muda mrefu pindi matokeo yanapokuwa mabaya.

 

Baada ya mchezo huo, Sarri alinu-kuliwa akisema: “Nahisi kuch-anga-nyikiwa, siko katika presha, sikuona kile nilichowa-fundisha ndiyo maana nachanga-nyikiwa.

 

“Yaweze-kana ni makosa yangu, labda nimeshindwa kuwaha-masisha, lakini timu yangu ni imara na inaweza kushinda hata kama hakuna kocha.”

 

Wakati wa mchezo huo mashabiki wa Chelsea walikuwa wakiimba na kumwambia Sarri hajui anachokifanya.

 

Inadaiwa kuwa baada ya mchezo huo, Sarri alitumia dakika 50 akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akizungumza na wachezaji wake, ambapo aliwaondoa wasaidizi wake wote na kubaki yeye na wachezaji tu wakizungumza.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.