KIBITI: Mwanamke Aliyejeruhiwa Kibiti Anatibiwa Hospitali, Hajafa!

KIBITI: Mwanamke aliyejeruhiwa kwa risasi usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Tabia Mbonde anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mchukwi, kinyume na taarifa zilizoenea kwamba amefariki.
Awali iliarifiwa kuwa watu wasiojulikana walimuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia juzi na kumjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu ambaye alikimbizwa hospitali kwa matibabu.
Global Publishers ilifunga safari mpaka hospitalini hapo na imefanikiwa kumpata majeruhi huyo ambaye alishuhudia mumewe akiuawa kwa risasi na yeye kukimbilia msituni baada ya kupigwa risasi tano mguuni.
Baada ya tukio hilo, mama huyo anadai alianguka msituni ambako alikuja kuchukuliwa na Wasamaria wema na kupelekwa hospitali.
Mama huyo amefunguka mengi kuhusu mauaji hayo ambayo utayapata kupitia Global TV Online na Gazeti la Risasi Jumamosi hii.
 
			
