The House of Favourite Newspapers

Kichuya Amchomoa Tambwe Ufungaji Bora

0
Shiza Kichuya

WINGA wa Simba, Shiza Kichuya amesema ni ngumu kwa Amissi Tambwe wa Yanga kuwa mfungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwani amekosa mechi nyingi pia bado ni majeruhi.

 

Hadi sasa imeshapita michezo tisa ya ligi kuu huku wikiendi hii ikitarajiwa kupigwa kwa kumi, ambapo hadi sasa Tambwe hajafunga hata bao moja pia hajacheza hata mechi moja akiuguza jeraha la goti.

 

Kichuya mwenye mabao matano ameliambia Championi Jumamosi kuwa, ni ngumu kwa Tambwe kuibuka

mfungaji bora msimu huu kwani bado hajapona na hata akipona atahitaji muda kukaa sawa.

Amissi Tambwe

“Unajua kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa sana kwa washambuliaji ambapo kila mmoja anakitolea macho kiatu cha ufungaji bora, kila mtu anajitahidi kufunga ili aweze kulifanikisha suala hilo.

 

“Ni ngumu kwa Tambwe kuwa mfungaji bora kwa sababu ameshakosa mechi tisa kwa sababu ya majeraha na hata akirejea haitakuwa rahisi kutukuta kwenye idadi hii ya mabao.

 

“Akirudi uwanjani, Tamwe atahitaji siku kadhaa za kurudisha makali yake sasa hapo na sisi tutakuwa tunapambana tufunge zaidi kwa hali hii naona haitakuwa rahisi awe mfungaji bora,” alisema Kichuya.

Leave A Reply