The House of Favourite Newspapers

Kidoa akwapua mume wa mtu

0

Kidoa (2)Asha Salum ‘Kidoa’ na anayedaiwa kuwa mme wa mtu wakiwa katika pozi.

Stori:  Hamida Hassan na Mayasa MaRiwata

Staa anayeibukia, Asha Salum ‘Kidoa’ wiki hii anatengeneza habari baada ya kudaiwa kuwa, hivi karibuni alikwapua mume wa mtu na kwenda kula naye bata huko Dubai.

Chanzo makini kilicho karibu na Kidoa kililitonya Ijumaa kuwa, Video Queen huyo kwa sasa amegombana na mpenzi wake aitwaye Mussa Masood ambaye alikuwa akimgharamia kila kitu kisa kikiwa ni safari ya Dubai ambapo alikwenda na mume wa mtu aliyefahamika kwa jina la Haidari.

“Hivi mnajua kuwa Kidoa na Mussa kwa sasa si wapenzi tena? Kama hamjui, habari ndiyo hiyo. Wamezinguana baada ya Kidoa kwenda kula bata na mume wa mtu anayeitwa Haidari,” kilidai chanzo hicho.

Kidoa (4)Baada ya habari hii kutua Ijumaa mwandishi alimtafuta Mussa ambaye alifunguka: “Dah! Sijui nianzie wapi lakini ukweli Kidoa amenikata stimu, sina hamu na mwanamke, nimemgharamia sana mpaka niliingia shoo room kununua gari kwa ajili yake lakini kumbe niliingia chaka.”

Musa aliongeza kuwa, siku kadhaa zilizopita walitofautiana kidogo lakini akashangazwa na taarifa kuwa, mchumba wake huyo alionekana akiwa na mwanaume aitwaye Haidari maeneo ya Sinza jijini Dar.

Kidoa (5)“Nilimpigia simu na alipopokea alikataa kuwa na mwanaume huyo, akanitajia msichana ambaye yuko naye wakati ni uongo.

“Sikujali niliendelea na kazi zangu lakini baada ya siku mbili niliona Kidoa akiwa ametupia picha yuko Dubai na hiyo ni baada ya kumpigia simu hapatikani, nilipopeleleza niliambiwa amekwenda na Haidari ambaye namjua ni mume wa mtu, nahisi mpaka sasa yuko naye,”  alisema Mussa.

Kidoa (3)
Baada ya Mussa kufunguka hayo, mwandishi wetu alimwendea hewani Kidoa ambaye alikuwa na haya ya kusema:

“Du! Huyo Mussa nilimuacha siku chache kabla sijaenda Dubai na huyo mwanaume anayenitajia simjui, nilienda na mtu mwingine,” alisema Kidoa.

Leave A Reply