The House of Favourite Newspapers

Kidoa Amkingia Kifua Mobeto

0
     Asha Salum ‘Kidoa’

MUUZA nyago matata Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’, amewataka mastaa wa kike Bongo waache kuendelea kumuandama mwanamitindo, Hamisa Mobeto baada ya kuzaa na Mbongo Fleva ambaye ni mzazi mwenza wa mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, kwani jambo hilo linamuathiri kisaikolojia.

Mwanamitindo, Hamisa Mobeto.

Akibonga na Star Mix, Kidoa ambaye anashikilia Taji la Ijumaa Sexiest Girl 2015 alisema kuwa, jambo ambalo linamstajabisha ni kitendo cha mastaa wengi Bongo kumsapoti Zari na kumponda Hamisa, kana kwamba hawamjui ilihali ni Mbongo mwenzao.

“Siyo sawa wasanii wenzangu wanavyomnyanyapaa Hamisa, kutwa kumpiga vijembe, wanapaswa kukumbuka kuwa hakuna ajuae kesho yake, huenda hata yeye hakuwaza kama yangemfika hayo,” alisema Kidoa

Leave A Reply