The House of Favourite Newspapers

Kiduchu yamrejesha Mike Tee

0

mike-teeMsanii mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’.

Umemmisi! Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva, Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’ amerejea ulingoni akiwa na ngoma mpya ya Kiduchu, aliyoiachia hivi karibuni.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Mike Tee ambaye alitamba na singo nyingi ikiwemo Sintobadilika, alisema kazi hiyo imepikwa katika Studio ya B2B chini ya Prodyuza Andrew Beatz na tayari iko hewani.

“Ngoma ya Kiduchu ni ya kwanza mwaka huu inayomzungumzia binti niliyekutana naye na ninamuomba anipe nafasi ya kummwagia mbwembwe zangu, nimejaribu kurejesha mawazo ya kiutu uzima ili kuwaonesha vijana kuwa bado niko vizuri,” anasema Mike Tee.

Leave A Reply