KIDUME AJITOSA KUZAA NA WEMA

BAADA ya mwigizaji bei mbaya Bongo, Wema Sepetu kusaka mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio, kidume cha mbegu, amejitokeza na kuapa kumzalisha staa huyo maarufu pia kwa jina la Tanzania Sweetheart.

 

Historia inaonyesha kuwa, Wema kwa nyakati tofauti amekuwa katika uhusiano na wenzi kadhaa na akionyesha nia ya kupata mtoto, lakini ilishindikana.

Kuna wakati alipokuwa na uhusiano na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliripotiwa kuwa na mimba, lakini baadaye ikadaiwa kuchoropoka.

 

KIDUME MWENYEWE NI NANI?

Kidume anayetajwa katika stori hii ni mpiga picha, mwongozaji na mwigizaji wa Bongo Muvi, Farid Uwezo.

Chanzo chetu cha habari kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, kimetueleza kuwa Farid na Wema ni marafiki wa karibu kwa muda mrefu, lakini Farid amekwenda mbali zaidi na kutaka kuoana na staa huyo wa filamu za Kibongo ambaye alitolewa na Filamu ya A Point of No Return aliyocheza na marehemu Steven Kanumba.

 

Sinema hiyo ilikuwa chanzo cha wawili hao kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, ambao baadaye ulivunjika na Wema kuingia kwenye penzi la mjasiriamali Jumbe Ismail.

“Nyie hamjui tu lakini nawatonya, Farid ana nia ya kumuoa Wema na ameshasema mara nyingi kuwa lazima amuoe,” kilieleza chanzo hicho na kuongeza:

“Mara nyingi hata kwenye mitoko huwa wanakuwa pamoja, fuatilieni mtajua ukweli.”

FARID ABANWA, AFUNGUKA

Risasi Jumamosi katika kujiridhisha, lilimvutia waya Farid na kumueleza kuhusiana na madai hayo, ambapo alifunguka bila kumung’unya maneno.

 

“Katika hilo mimi nitakuwa mkweli kabisa, nampenda sana Wema kwa moyo wangu wote na nipo tayari kuishi naye. Mimi siyo kama watu wengine wa longolongo, nataka kupeleka barua kwao, nitoe na mahari nimuoe jumla.

“Siwezi kusema uongo mwezi huu wa Ramadhan, nia yangu ni ya dhati. Kuna wakati niliwahi kumwambia lengo langu, akachukulia poa, akanijibu tu: ‘Inshallah’ lakini ukweli ndiyo huo. Nipo serious katika hili,” alisema Farid.

 

AZUNGUMZIA KUZAA NAYE

“Nimeshasikia mengi, sina haja nayo. Ninachojua mimi ninampenda na akinikubalia kweli nitamuoa na kuzaa naye watoto. Hayo mambo ya skendo ni historia, sina haja nayo.

 

“Amepitia mengi, ameandikwa kwa mengi. Yapo ya ukweli na mengine ya kutunga lakini kwangu siyo ishu, ninachoangalia ni moyo wangu unavyosema dhidi yake. Kwa kweli nampenda sana Wema.

“Ngoja niweke mambo yangu sawa, nipeleke posa kwa mama yake. Wallah nikikubaliwa, kinachofuata ni mahari na kuvuta jiko langu ndani,” alisema Farid.

 

WEMA KICHEKO

Baada ya kumalizana na Farid, Risasi Jumamosi lilimgeukia Wema ambapo lilimpigia simu na kumweleza mtiririko wa stori nzima, Wema akaangua kicheko cha nguvu, kisha akasema:

 

“Farid huyuhuyu ninayemjua…. ha ha ha, labda anatania bwana. Anataka kunioa mimi? Hawezi kufanya hivyo bwana… ngoja tuone,” alisema Wema akiendelea kucheka, kisha akakata simu.

Risasi Jumamosi linaendelea kufuatilia ishu hii kwa undani ili kuona mwisho wake, tunaahidi kuwahabarisha kitakachotokea.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

Alichokisema Waziri MKUU Kwenye Fainali za Mashindano ya Quraan


 

Loading...

Toa comment