KIDUME ALIYEFUFUKA AFARIKI TENA

 

MWANAMME  wa Ethiopia ”aliyefufuka” wakati wa mazishi yake miezi mwili iliyopita amefariki dunia tena.

 

Hirpha Negero alithibitishwa kufa mwezi Novemba mwaka jana ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akiligonga jeneza hilo.

 

Hirpha alilisimulia shirika la utangazajila Uingereza (BBC) yaliyomfika wakati huo kamba, ”Nilisikia mtu akilia. Nilijihisi kuishiwa na pumzi ndipo nikajaribu kujitoa katika hali hiyo. Nilikuwa mnyonge, hata sikuweza kuzungumza,” anasema na kuongeza kwamba alifanikiwa kuita watu.

“Hapakuwa na mtu yeyote karibu?” mchimba kaburi, Etana Kena, anasema watu walishtushwa na tukio hilo na wote walikimbia na kuliacha jeneza, hivyo ilibidi ajifungulie mwenyewe.

 

Baada kisa hicho hafla ya maziko iligeuka kuwa sherehe.  Kena ambaye pia ni mjomba wa Hirpha alisema: “Nimezika zaidi ya miili hamsini au sitini. Sijawahi kushuhudia maajabu kama haya. Alionekana kama amefariki.”

 

‘Marehemu’ huyo alisema kuwa aliona mahali pazuri sana wakati alipokuwa amepoteza fahamu, ambapo mwanamme aliyekuwa amevalia nguo nyeupe alimwambia ”rudi nyumbani”.

 

Dkt.  Birra Leggese ameliambia BBC, huenda Hirpha alipoteza fahamu kwa kiwango cha juu sana (deep coma).

 

Hata hivyo, mchimba kaburi huyo wa awali alimzika tena Hirpha kwa mara ya pili siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake.

 

Alisema: “Mara hii nilikuwa na hakika amefariki kwa sababu nilishuhudia jinsi alivyougua kwa muda mrefu.”

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Toa comment