The House of Favourite Newspapers

Waandamana Kudai Haki Katika Kifo cha Mfaransa Mweusi

0



WAANDAMANAJI zaidi ya 20,000 wamekusanyika jijini Paris, Ufaransa,  kudai haki itendeke katika kifo cha Mfaransa mweusi, Adama Traore (24), aliyefia mikononi mwa polisi mwaka 2016

Uchunguzi wa mazingira ya kifo cha Traore umekuwa ukiendelea kwa miaka takriban minne huku kukiwa na ripoti zinazopingana kuhusu kile kilichosababisha kifo chake. Kisa cha Traore kimekuwa ushahidi mkubwa kuonyesha ukatili unaofanywa na polisi nchini humo.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni imedai chanzo cha kifo chake ni matatizo ya moyo lakini familia yake inadai kwa mujibu wa uchunguzi binafsi waliofanya, alifariki kutokana na kushindwa kupumua kutokana na namna alivyodhibitiwa na polisi.

Polisi jijini Paris wametumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji hao waliokuwa wanapinga ubaguzi wa rangi na ukatili unaofanywa maafisa wa polisi

Maelfu ya wananchi walikusanyika kwenye maandamano hayo na kukiuka agizo la kuepuka mikusanyiko lililowekwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Mbali na kutaka haki kwenye kifo cha Traore, pia walikusanyika kama ishara ya umoja kuunga mkono maandamano ya kifo ya Mmarekani mweusi,  George Floyd, aliyefariki baada ya polisi kumkandamiza kwa goti shingoni.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa jiji la Paris, Didier Lallement, ametetea kikosi chake dhidi ya tuhuma za ubaguzi na ukatili.

Leave A Reply