The House of Favourite Newspapers

Kifo Cha Ndiku Chamshindisha Ndani Sasha

0
Muuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Sasha Kassim.

MUUZA nyago kwenye video za Bongo Fleva, Sasha Kassim amefunguka kuwa, alipata mshtuko mkubwa baada ya kusikia taarifa ya kifo cha aliyekuwa msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ hivyo kujikuta akishinda ndani kwa kukosa ‘mudi’ ya kufanya mishemishe zake za ‘tauni’.

Hamad Ndikumana ‘Katauti’.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Sasha alisema kuwa, tangu zamani, akiwa anasoma alikuwa akiipenda familia ya Ndikumana na mkewe, Irene Uwoya ambaye ni staa wa Bongo Movies hivyo alivyosikia kuhusu kifo hicho aliumia mno.

 

“Katika ‘kapo’ niliyokuwa ninaipenda tangu nikiwa ninasoma ni ya Ndikumana na Irene. Nilikuwa napenda kuwasoma kwenye vyombo vya habari. Kiukweli kifo chake kimeniumiza mno,” alisema Sasha. Ndikumana alifariki dunia wiki mbili zilizopita kwa kile kilichoelezwa kuwa kifo chake kilisababishwa na matatizo ya moyo.

Leave A Reply