The House of Favourite Newspapers

Kigogo adaiwa kuvunja penzi la Malaika

0

MALAIKAImelda Mtema

KIGOGO mmoja wa serikalini anadaiwa kutibua penzi la Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ na mpenzi wake wa siku nyingi (jina linahifadhiwa) na kwamba wameshaachana.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na msanii huyo, mara nyingi Malaika alikuwa akichelewa kurudi nyumbani akitokea kwenye vikao alivyokuwa akivifanya na watu wa serikalini kuhusiana na muziki wake.

“Kitendo hicho kilimchukiza sana mchumba wake kwani alipogundua tu kuwa anazungukwa na kudanganywa aliamua moja kwa moja kumtema Malaika,” kilisema chanzo.

Baada ya mtandao huu kupata ubuyu huu, lilimtafuta Malaika kwa njia  ya simu ambapo alisema kuwa hizo habari hata yeye amezisikia lakini hazina ukweli wowote.

“Hizo habari nimezisikia sana zikivuma, lakini mbona nipo poa tu na mpenzi wangu! Hakuna ukweli wowote hapo,” alisema Malaika.

Leave A Reply