The House of Favourite Newspapers

Kigogo Msd Aachiwa Huru na Mahakama

0

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki Byekwaso Tabura leo Mei 13, 2021 wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

 

Wameachiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20 iliyofanyiwa maitio mwaka 2019. Ambacho kinampa mamlaka DPP kuondoa kesi mahakamani wakati wowote.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele baada ya wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon kuwasilisha mahakamani hapo hati ya kuwafutia mashtaka (Nolle Prosequi) washtakiwa iliyosainiwa na aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga Mei 10,2021 akionesha kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo utakatishaji fedha haramu zaidi ya Sh bilioni 1.6.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ilidaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar wa Salaam wakiwa watumishi wa umma kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Inadaiwa Bwanakunu akiwa ni mtumishi wa umma alifanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kongeza mishahara na posho za wafanyakazi bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi na kuisababishia MSD hasara ya Sh Sh 85,199,879.65.

 

Leave A Reply