The House of Favourite Newspapers

Kigwangalla Aongoza Siku ya Takwimu Afrika

kigwangalla-1Naibu Waziri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, akihutubia katika hafla hiyo.

Dar es Salaam: NAIBU Waziri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, leo ameongoza watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Dk.  Kigwangalla aliongoza hafla hiyo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Phillip Mpango aliyekuwa ametarajiwa kuwa mgeni rasmi.

kigwangalla-2Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk.,Albina Chuwa, akisoma hotuba yake.

Maadhimisho hayo yameanza majira ya saa tatu asubuhi ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya takwimu na wananchi wamejitokeza kwa wingi.  Maadhimisho hayo yanalenga kuongeza uelewa mpana kwa watumiaji wote wa takwimu Afrika kuhusu umuhimu wake katika kupanga mipango ya maendeleo katika sekta zote za kijamii na kiuchumi barani Afrika.

kigwangalla-3

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho hayo.

Akizungumza  katika hafla hiyo Dk Kigwangalla alisema siku hiyo inayoadhimishwa  kila mwaka ilianzishwa  na Bodi ya Taifa ya Takwimu Barani Afika ambapo hutolewa mada mbalimbali kuhusu elimu ya matumizi bora ya takwimu ndani na nje ya nchi.

kigwangalla-4Baadhi ya wanafunzi waliofika kwenye maadhimisho hayo.

Alifafanua kuwa maadhimisho hayo ni muhimu katika kupanga maendeleo na kutunga sera katika bara la Afrika hususani wanafunzi wa shule za sekondari na wanavyuo wanaosomea mambo ya takwimu katika kujifunza tathmini na kufuatilia malengo katika mipango ya maendeleo na mambo mbalimbali yanayohusu takwimu.

kigwangalla-5Hafla ikiendelea.

Kauli mbiu ya siku hiyo mwaka huu 2016 ni  “Kuimarisha Takwimu za Kiuchumi kwa Mtangamano wa Kikanda, Mabadiliko ya Miundo na Maendeleo Endelevu”.

 Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.