Na Denis Mtima/GPL
NAIBU Waziri katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangallah, leo ameongoza wakazi wa jijini la Dar katika maadhimisho ya Siku ya Ustawi wa Jamii ambayo yamefanyika katika viwanja vya Taasisi ya Chuo cha Ustawi wa Jamii eneo la Mwenge-Bamaga.
Maandamano yalianzia Viwanja vya Zahanati ya Mwenge na kuhitimishwa katika viwanja vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ambapo waziri huyo alitembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho ya huduma za wataalamu wa ustawi wa jamii na kazi za wateja na wadau mbalimbali.
Comments are closed.