The House of Favourite Newspapers

Kihenzile Ashuhudia Makabidhiano ya Jengo Jipya la Abiria Kahama Airport Kutoka Kampuni ya Dhahabu ya Barick

0
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile ameshuhudia makabidhiano ya jengo jipya la abiria Kahama Airport kutoka kampuni ya dhahabu ya Barick kwenda kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA).
Jengo hilo lina thanani ya Tsh. milioni 896.7 na litahudumia abiria 200 ikilinganishwa na abiria 25 hapo awali.
Limekabidhiwa na Mtendaji Mkuu na Rais wa Barick, Mark Bristow ambapo Viongozi mbalimbali wameshiriki katika hafla hii ikiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christine Mdeme, Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof Godius Kahyarara na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Ndg Hamis Rashida Amir.
Leave A Reply