The House of Favourite Newspapers

Kijana Aliyeokoa Abiria wa Ajali ya Ndege ya Precision Air Apewa Zawadi

0
Miili ya marehemu 19 ikiwa inaagwa katika Uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba

SERIKALI kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila imempongeza kijana Majaliwa Jackson aliyeokoa Maisha ya abiria 26 waliopata ajali kwenye ndege ya Shirika la Precision Air kwa kumpatia kiasi cha shilingi milioni moja (1).

 

Akiongea katika Hafla ya kuaga miili ya marehemu waliopata ajali RC Chalamila amempongeza kijana huyo kwa ujasiri na uzalendo aliouonesha wa kuokoa Maisha ya wahanga hao wa ajali.

Kijana Majaliwa amepewa zawadi ya shilingi milioni moja kama pongezi kwa juhudi zake za uokoaji lakini pia amepewa shilingi milioni 2 kutoka Shirika la Precision Air

Hadi sasa takwimu rasmi imeonesha ni jumla ya watu 19 wamefariki na Serikali pamoja na mashirika na taasisi binafsi zinaendelea na juhudi za kuhakikisha familia za wafiwa zinapata msaada wa kushikwa mkono katika kipindi hiki kigumu.

 

Aidha Shirika la Usafirishaji la Precision Air limetoa kiasi cha shilingi milioni mbili (2) kwa kijana Majaliwa kama sehemu ya pongezi kutokana na juhudi alizozionesha kwenye uokoaji wa wahanga hao wa ajali.

 

Naye Katibu Mkuu wa NEC taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka  amewataka wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa wavumilivu na kubainisha kuwa Chama cha Mapinduzi kupitia kwa Mwenyekiti wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

Leave A Reply