The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kikwete: Jana Nilikuwa na Mkapa, Kifo Siri ya Mungu – Video

0

RAIS wa awamu ya nne,  Jakaya Kikwete amesema hali ya kiafya ya rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin  Mkapa,  haikuwa mbaya alipoenda kumuona jana jioni hospitali.

 

Amesema hayo alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mkapa kujumuika na ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania katika maombolezo ya kiongozi huyo ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Julai 24, 2020.

 

“Jana jioni nilikwenda kumuona hospitali. Tulizungumza sana kwa karibu saa moja. Alikuwa na maumivu ila si yale maumivu ya kutoka kumuona mgonjwa na kumwambia mwenzako nimemuona mgonjwa ila eenhe!

 

“Nilipopata taarifa usiku wa manane kwamba mzee amefariki niliuliza kumetokea nini tena, kwa sababu hakuwa mgonjwa wa kutia shaka na niliondoka nikamuaga kwamba nitakuja kukuona kesho ila siombei uendelee kukaa hospsitalini, tuonane nyumbani.

 

“Kifo ni siri ya Mwenyezi Mkungu. Ila kubwa ni kwamba tumepoteza moja ya viongozi mashuhuri, mkuu wa nchi yetu aliyetumikia taifa letu vizuri kwa uadilifu mkubwa na moyo wa upendo. Nawaomba Watanzania kuwa na moyo wa ustahimilivu na uvumilivu.

 

“Niwaombe Watanzania katika kipindi hiki tuendelee kuomboleza kifo cha Mzee Mkapa, tuwe na moyo wa subira na kukubali kuwa kifo kimeumbwa na Mungu, wote ni Wwtu wake na kwake tutarejea, sasa tutarejea lini hiyo ni siri yake mwenyewe Bwana Mkubwa aliyetuleta duniani.

 

“Tumepoteza mtu ambaye amelitumikia taifa letu vizuri, kwa heshima na uadilifu mkubwa, la kuomba tu kwa Watanzania katika kipindi hiki ni kuendelea kuomboleza na kuwa na moyo wa subira kukubali tu kwamba kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu kila mmoja ndiyo njia yake.

 

“Tumkumbuke kwa mengi aliyoyafanya na tuhakikishe yale aliyoyasimamia na kuyapigania katika kipindi chote, tuyaendeleze kwa manufaa ya taifa letu,” amesema Kikwete.

Leave A Reply