The House of Favourite Newspapers

Kilichotokea Mahakamani Kesi ya ‘Mpemba wa Magufuli’

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Ali maarufu ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake kwa sababu mawakili wao hawakuwepo.
Wakili wa Serikali, Elia Athanas, amemuambia, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya uamuzi. Hata hivyo, washitakiwa hao walikuwepo mahakamani hapo ambapo Hakimu Simba amesema kwa sababu hiyo anaahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21, mwaka huu.
Washtakiwa hao ni miongoni mwa washitakiwa waliomuandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba kukiri mashitaka yao. Katika kesi hiyo, mbali ya Mpemba washitakiwa wengine ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chima, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno tembo yenye thamani ya Sh. Mil. 785.6.
Pia inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Tsh. Mil. 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Comments are closed.