The House of Favourite Newspapers

Kilichowakuta Wahamiaji Hawa Mikononi mwa Muroto, Hawatasahau!

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia Raia wanne kutoka nchini za Somalia na Ethiopia Kwa kuingia nchini bila kibali huku pia likiwashikilia watu wawili Raia wa Tanzania waliokuwa wakiwasafirisha wahamiaji haramu hao.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Okt.24,2019 jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Girres Muroto amesema mnamo tarehe 23,10,2019 majira ya saa 10:00 huko katika kijiji na kata ya MTERA Tarafa ya RUDI Wilaya ya MPWAPWA Mkoani Dodoma ,walikamatwa wahamiaji haramu wanne walioingia nchini bila vibali.

 

Kati yao ,Wawili ni Raia wa Ethiopia na Wawili ni Raia wa SOMALIA huku pia wakikamatwa watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha wahamiaji haramu hao kutoka ARUSHA Kwenda IRINGA kwa Kutumia Usafiri wa pikipiki mbili.

 

Waliokamatwa ni Sellamu Yohanes[24] Raia wa Ethiopia,Ashetu Tesfaye[20]Raia wa Ethiopia,Mahamoud Mapaa[19]Raia wa Somalia, Cuse Ciise [18]Raia wa Somalia.

 

Kamanda Muroto amewataja Raia wa Kitanzania waliokuwa wakiwasafirisha wahamiaji haramu hao kwa kutumia pikipiki ni Jamali Babuu Martin [26] dereva wa bodaboda ,mkazi wa ORASITE ARUSHA akiendesha pikipiki namba MC 942 AXK KINGLION Chassis Na.LTBPK8BG5F2KO9729 rangi nyeusi.

 

Mwingine ni Wiston Alex MAKIA ALLY [25] Dereva wa Bodaboda mkazi wa Mbauda ARUSHA akiendesha pikipiki Na.MC 767 CEB DAYUN Chassis Na.L7GPCJLYH1099156 rangi nyeusi.

 

Kamanda Muroto ametaja mbinu waliyotumia kuingia nchini ni kwa kutumia usafiri wa pikipiki kuvuka mipaka na vizuizi vya barabarani.

 

Aidha, amebainisha kuwa watuhumiwa walijaribu kuwarubuni askari kwa kutoa rushwa ya Tsh. Milioni moja [1,000,000/=] ili waweze kuachiliwa na wakati wanakamatwa walikuwa na pesa Tsh.laki tano[500,000/=] lakini askari walikataa hongo ya rushwa hiyo na waliwakamata pamoja na pesa yao na kuwafikisha kituoni na watafikishwa mahakamani.

 

Katika hatua nyingine kamanda Muroto amesema Jeshi hilo limekamata nyara za Serikali ambapo mnamo Tarehe 21,10,2019 majira ya saa 1:30 jioni huko kijiji na kata ya MKOKA Tarafa ya ZOISA Wilaya ya KONGWA Mkoani Dodoma alikamatwa STEPHANO MTAGWA KOGANI[39] Mkazi wa kijiji cha SONGAMBELE na HAMIS MATHAYO MABUKU [45] na mkazi wa kijiji cha MATONGOLO Wakiwa na pembe moja ya tembo ndani ya mfuko wa Salfeti kiroba kinyume cha sheria na watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

 

Tukio jingine Kamanda Muroto amesema ni la kuvunja nyumba mchana na kuiba ambapo amekamatwa ELIAS SHABAN JOSEPH [21]Mkazi wa Mailimbili Mnadani baada ya kuvunja nyumba mchana na kuiba maboksi 8 ya mafuta ya kupaka na maboksi 4 ya pipi mali yenye thamani ya TSH.720,000 Maeneo ya IPAGALA WEST Dodoma mali ya Willy Fidelis Mgeni huku pia wakikamatwa wengine walioshiriki uhalifu huo

 

Hata hivyo,Kamanda Muroto ameipongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuuhabarisha umma.

Comments are closed.