The House of Favourite Newspapers

Kilima Chenye Maajabu Kiendacho kinyume na Sheria za Mvutano

0
Katika kilima hiki vyombo vya usafiri huserereka wakati wa kupanda

KILIMA hiki cha mvutano ni kilima kinachofahamika kuwa cha ajabu, kwa kuwa kinatengeneza kiini macho kupelekea watu kuhisi kama vile gari iliyoachwa kwenye gia inaserereka kupanda mlima kwa kwenda juu wakati ni kitu ambacho sio sawa kwa kuzingatia sheria za asili ya mvutano, japo watu wengine wanaamini kwamba ni kilima chenye sumaku lakini hata ukiweka kitu kisicho cha chuma kama mpira pia huishia kuserereka kwenda juu ya kilima hicho.

 

Kuna maelfu ya vilima vya mvutano duniani na watafiti katika Chuo kikuu cha Padova na Pavia huko Italy, waligundua kuwa bila kuwepo na upeo wa macho wa kweli inakuwa ngumu kwa mtu kuhukumu uso wa mteremko, hivyo basi kama rejeo linaloaminika linakosekana basi hata vitu huonekana kama vile vimeinama mfano mzuri ni kama miti.

Kibao cha ishara ya kilima hicho

Kilima kama hicho hupatikana moja wapo ya nchi ya Scotland kusini Ayrshire, kiitwacho kwa jina la The Electric Brae, kama vilima vingine kilima hiki pia kilichopo Scotland, kina sifa hizo za kufanya magari kuonekana yakiserereka kwenda juu ya kilima wakati yakiwa kwenye gia, haya maajabu yamevutia sana watalii kutoka nchi mbali mbali na imewabidi kutembelea na kujionea kwa macho yao wao wenyewe.

 

Jina hilo la The Electric Brae lilopewa kilima cha Scotland, ni jina lilofikirika kwa sababu ya kudhani kuwa matukio hayo yalikuwa yakisababishwa na umeme ama mvuto wa sumanku kwenye Brae, jina hilo lilianza kugaiwa kwa miteremko mingine ya huko Scotland.

 

Ni ngumu sana kupata jawabu juu ya matukio hayo, sababu imekuwa kila mtu ana mawazo yake juu ya maajabu hayo kama vile wengine wanaita ni mvutano wa kilima (gravity-hill), na wengine kwa urahisi wanasema kuwa ni sababu ya mvuto wa sumanku, haijulikani ni majina gani sahihi ya kuita matukio haya yanayotokea katika vilima hivyo vya maajabu.

 

Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem Kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply