The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Akina Halima Mdee, Mwaifunga Ashindwa Kutoa Ushahidi

0
Aliyekuwa Makamu mwenyekiri wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) Hawa Mwaifunga, ameshindwa kutoa ushahidi wake baada ya kuieleza Mahakama kupitia kwa wakili wake kuwa anaumwa.
Mbunge huyo ni miongoni mwa  wabunge wenzake 18 waliofungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).
Mbunge huyo ameieleza mahakama kupitia kwa jopo la mawakili wake wakati wa kikao cha majadiliano mafupi baina ya mawakili wa pande zote na jaji anayesikiliza kesi hiyo,Cyprian Mkeha, kuwa anaumwa na kwamba anasumbuliwa na mgongo.
Kutokana na taarifa hiyo Jaji Mkeha ametoa uamuzi wa kuiahirisha kesi hiyo katika kikao hicho bila kuingia mahakamani na kisha mawakili wa pande zote wakatoa taarifa hizo kwa wateja wao wanaowawakilisha.
Kiongozi wa jopo la mawakili wa Chadema, Peter Kibatala na Kiongozi wa jopo la mawakili wa kina Mdee, Ipilinga Panya kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kesi hiyo itaendelea tena Novemba 3 na 4, 8 na 9 na Desemba 6 na 7, 2022.
Siku hiyo Mwaifunga ataendelea na ushahidi wake aliouanza tangu Oktoba 13, mwaka huu.
Leave A Reply