The House of Favourite Newspapers

KIM NANA AWASHANGAA WANAWAKE WADANGAJI !

Tokeo la picha la Lilian Kessy, ‘Kim Nana’
Lilian Kessy, ‘Kim Nana’

MWANAMITINDO Lilian Kessy, ‘Kim Nana’ amesema, anawa-shangaa baadhi ya mastaa wanao-danga mjini na kushindwa kutumia fursa zilizopo kujipatia fedha.  Akiongea na Risasi Jumamosi, Kim alisema kuwa anawashangaa wasichana wengi hasa mastaa wanaodanga wakati fursa za biashara zipo nyingi na mbali na biashara kazi za kufanya zinapatikana.

“Unajua sisi ambao tuna majina tayari yawe makubwa au madogo ukijaribu kitu kushindwa ni ngumu sana hivyo mimi nawashauri wanaodanga wabuni hata miradi au wajitokeze kwenye makundi yanayofunza ujasiriamali watatoka tu kimaisha,” alisema Kim Nana.

Kim ametokea kwenye U-video Quee ambapo ameonekana kwenye nyimbo za wasanii mbalimbali lakini pia ameweza kujiajiri mwenyewe kwa kutengeneza mavazi kwa lebo yake ambayo inaendelea kufanya vyema.

Comments are closed.