The House of Favourite Newspapers

Kimbunga Hilary kugonga California mwishoni mwa wiki kikitokea Mexico

0

Kituo cha kitaifa cha vimbunga hapa Marekani kimesema Alhamisi kwamba kimbunga Hilary kimeongeza kasi na kufikia kiwango cha pili karibu na ufukwe kwa Mexico wa Pacific, kikitarajiwa kusababisha mvua kubwa kusini magharibi mwa Marekani kufikia mwishoni mwa wiki.

Taarifa zimeongeza kusema kwamba Hilary kina upepo wa kilomita 165 kwa saa na huenda kikagonga ufukwe wa Baja kwenye penisula ya California kufikia mwishoni mwa wiki.

Hilary kilionekana takriban kilomita 805 kusini- kusini mashariki mwa Los Cabos kwenye upembe wa kusini mwa peninsula ya Baja. Ingawa kilikuwa mbali na nchi kavu, kililikuwa kilielekea magharibi – kaskazini magharibi kwa kasi ya kilomita 22 kwa saa, huku kikitarajiwa kugeuka upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Marekani.

Kulingana na idara ya kitaifa ya hali ya hewa ya Marekani, hakuna kimbunga kigingine kilichofika kusini mwa California tangu Septemba 25, 1939.

RC CHALAMILA HAJAWAHI KUKASIRIKA HIVI – ”ZOMEEENI MUONE, MUKOME KAMA MULIVYOKOMA KUNYONYA”…

I

Leave A Reply