The House of Favourite Newspapers

Kimenuka! Spika Ndugai Aicharukia Serikali Sakata la Mafuta – Video

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemhoji Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kuhusiana na suala la meli mbili za mafuta yanayodaiwa kuwa ni ghafi (Crude Oil) zilizokwama Bandarini kutokana na tozo ya ushuru.

 

Waziri Mwijage amesema mafuta hayo yana utata mkubwa kufuatia ripoti ya TRA kuwa ni mafuta ghafi au Safi, hivyo amemuomba Spika ampe muda mfupi baadaye saa 11 atarudi kutoa majibu.

 

Kufuatia majibu hayo, Spika amekubaliana na ombi hilo huku akisisitiza watumishi wa serikali kusimama kwenye ukweli, na kulipatia ufumbuzi suala hilo haraka iwezekanavyo kwani wanaoumia ni wananchi walaji.

MSIKIE NDUGAI AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.