The House of Favourite Newspapers

KINJE AMVUTA UWOYA KIMYAKIMYA, ATANGAZA BIFU NA DOGO JANJA

Kinje, Uwoya na Farid Uwezo
Kinje (wa kwanza kushoto) akiwa na wasanii wenzake location. Kulia kwake ni Bi Mwenda, Kabirigi na Farid Uwezo

Msanii wa filamu za Kibongo anayekuja kwa kasi kwenye gemu, Chriss Lubango ‘Kinje’, amemvuta msanii mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Irene Uwoya na kumshirikisha kwenye filamu yake iitwayo Kinje huku akilalamika kwamba msanii wa Bongo Fleva anayetajwa kuwa mwandani wa sasa wa uwoya, Dogo Janja amekuwa kikwazo cha wao kukamilisha kazi yao kwa wakati.

Kinje ambaye tayari ameshafanya kazi na mastaa kibao wa Kibongo, wakiwemo Aunt Ezekiel, Hamisa Mobeto na wengine wengi, amesema tayari kazi waliyoifanya na Uwoya imekamilika na kinachosubiriwa ni taratibu za kuizindua, ambapo amesema anaamini italeta mapinduzi makubwa ya sanaa Bongo.

“Ninachoomba ni mashabiki kuniunga mkono kwa sababu nipo kwenye gemu tangu 2011 natafuta njia ya kutimiza malengo yangu,” alisema Kinje.

Sehemu ya filamu hiyo itarushwa leo (Jumamosi) kupitia Global TV Online, namna ya kuitazama, ingia Youtube kisha andika Global TV Online, subscribe kisha utajiona filamu hiyo na video nyingine nyingi!

Comments are closed.