The House of Favourite Newspapers

Kipigo Cha Azam FC Chamuibua Lwandamina

0

KIPIGO cha mabao 2-1 walichokipata Azam FC kutoka kwa Klabu ya Coastal Union kimemuibua kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina huku akisema kuwa ubovu wa uwanja umechangia timu yake kushindwa kupata matokeo.

 

Azam FC baada ya kupoteza mchezo huo katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga timu hiyo sasa imeshindwa kupata matokeo katika michezo miwili mfululizo ya ligi kwani katika mchezo uliopita walitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Lwandamina alisema: “Tumepoteza mechi kutokana na uwanja ulivyo, ilikuwa ni ngumu kwetu mpira kutulia ukiwa chini, staili yetu ya kucheza ni ya kupiga pasi za chini lakini uwanja haukuwa rafiki kwetu, tutajitahidi tufanye vizuri katika michezo ijayo.

 

”Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Tumepoteza mchezo kutokana na ubora wa wapinzani wetu na mara zote tumekuwa tukipata wakati mgumu tunapokuwa katika uwanja huu, hivyo tunajipanga kufanya vizuri katika michezo ijayo.”

Leave A Reply