The House of Favourite Newspapers

Kipigo cha Mobeto, Diamond Amfananisha Mama Yake na Bondia Tyson

IKIWA ni wiki moja imepita tangu Mzazi mwenzake na Msanii Diamond Platinumz, Hamisa Mobetto achezea kichapo cha ‘Mbwa Koko’ kutoka kwa mama wa Msanii huyo, Bi. Sandrah, mapya yameibuka tena baada ya Diamond kutoa jibu la tukio hilo akimfananisha mama yake na Staa wa ngumi za kulipwa aliyewahi kutikisa dunia, Mike Tyson.

 

Diamond kupitia mitandao wa kijamii, ametupia comment kwenye video ya Mama ya aliyoiweka kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika maneno haya; “Tysoooooooon!!!!😅,” amecomment Diamond kwenye video hiyo.

Comments are closed.