The House of Favourite Newspapers

Kipindupindu Chalipuka Kilimanjaro, Watu 26 Walazwa

UGONJWA wa Kipindupindu umeripotiwa kuripuka mkoani Kilimanjaro ambapo wagonjwa 26 wamelazwa katika hospitali ya TPC huku eneo hilo likitengwa mahususi kwa kuhudumia wagonjwa hao.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema wagonjwa wengi wanatoka Wilayani Simanjiro huku ikielezwa kuwa mlipuko huo ni miongoni mwa athari zilizotokana na mafuriko katika maeneo mengi ya bonde la mto Pangani.

 

Maeneo yaliyoathirika zaidi kwa mkoa wa Kilimanjaro ni Chemchem, Kirungu, Mikocheni, Kahe na New land huku kwa upande wa Mkoa wa Manyara ni eneo lote la Msitu wa Tembo.

 

Aidha, ni nadra sana kwa Kilimanjaro kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na usafi uliopo katika mkoa huo.

Comments are closed.