KISA BWANA AKE MPYA, WOLPER AMUITA X- WAKE MUIMBA TAARAB

Bongo Muvi

Wolper Akiwa Na Mpenzi Wake Wa Sasa

POVU alilolitoa Diva anayetikisa kiwanda cha Bongo Muvi, Jacqueline Wolper kwa X- wake, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ni povu ‘hevi’, kiasi kwamba hata kama ni nguo chafu kiasi gani lazima zitatakata kwani amemuita ni muimba Taarab.

Kwa mujibu wa mashabiki, hasira za mkizi zilimkamata Wolper baada ya X- wake huyo kuwa anamfuatilia mara kwa mara kwenye 18 zake, kiasi cha kumsababishia mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina la Brown, kupaniki na kuhisi labda huenda, wawili hao bado wana uhusiano wa siri.

Bongo Muvi

Posti Ya Wolper Kwenye Ukurasa Wake Wa Instagram

Baada ya posti hiyo ya Wolper, mashabiki wakashusha komenti kibao. Wengine walimpongeza kwa kutoa kichambo hicho, wapo waliomkosoa na kumwambia kwa nini hizo siri hakuzisema kipindi walipokuwa pamoja, na wengine waliishia kusema kwamba mapenzi ya mastaa wa Kibongo ni ‘kizunguzungu’.

NA ISRI MOHAMED/GPL


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment