The House of Favourite Newspapers

Kisa mashabiki AS Vita, Wachezaji Simba Waonywa

Mashabiki wa AS Vita Club.

WACHEZAJI wa Simba wametakiwa kuelekeza nguvu zao nyingi katika mchezo wa leo na kuachana na kuwasikiliza mashabiki wa AS Vita Club ya hapa. Mashabiki wa Vita Club ni maarufu kwa kuwachanganya wageni wanaokuja kucheza katika Uwanja wa Mertyrs kutokana na wingi wao.

 

‘Wenyeji’ wa Simba wengi wakionekana ni mashabiki wa DC Motema Pembe wamekuwa wakiwasisitiza Simba kuachana kabisa na mawazo ya mashabiki.


“Wanachotakiwa wachezaji wa Simba ni kucheza mpira hasa. Wacheze kwa nguvu na kujituma na hakuna haja ya kuhofia kelele zao.

 

“Kelele zao ni nyingi sana, wako wengi sana lakini hawawezi kuingia uwanjani, haina haja ya kuogopa,” walisema mashabiki hao wakipokezana wakionekana wamelenga kuipa moyo Simba iwafunge wapinzani wao.

 

Mara nyingi mashabiki hao wa AS Vita Club hushangilia mwanzo mwisho huku baadhi wakijipanga nje ya uwanja kwa lengo la kutengeneza hofu kwa timu pinzani. DC Motema Pembe imekuwa na upinzani mkubwa na AS Vita Club na mara kadhaa mashabiki wao wamekuwa wakitwangana na ngumi bila ya kumpata mbabe kamili.

Comments are closed.