The House of Favourite Newspapers

TANZIA: TASNIA YA MUZIKI WA BONGO YAPATA PIGO

TASNIA ya Muziki wa Bongo leo imekumbwa na msiba baada ya aliyekuwa muimbaji wa Bendi ya Mapacha Musica, Erick Kantona, amefariki dunia kwa ajali ya gari katika maeneo ya Dawasco, Tegeta jijini Dar es salaam leo Jumamosi, Januari 26, 2019 asubuhi.

 

Kantona ambaye amekuwa maarufu kwa mahili wake wa kutunga na kuimba nyimbo za dansi, aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Mapenzi Kitu Gani’ ambao aliuimba na bendi ya Diamond Music kabla ya kuhamia Mapacha Watatu.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Erick mahala pema peponi, AMEN!

 

Comments are closed.