The House of Favourite Newspapers

Kisa Ndoa Yake, Uvumilivu Umefikia Kikomo, Dogo Janja Aanika Haya!

MSANII wa Bongo Fleva, Dogo Janja ‘Janjaro ambaye ni mume wa ndoa wa muigizaji wa Filamu Bongo, Irene Uwoya, amesema wimbo wake mpya wa ‘Wayuwayu’ ni dongo maalumu kwa watu waliokuwa wakiiponda ndoa yake bila kujua undani wao ulivyo.

 

Janjaro amesema hayo baada watu wengi kusema vibaya ndoa ya wawili hao kuwa hawaendani kwa kila kitu;

 

“Watu walikuwa wanakejeli na kuongea mambo kibao ili nionekane mimi kidagaa, sina chapaa, wananitukana lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu. ‘So’ wimbo wa Wayuwayu ulikuwa ni sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya watu na wala wasiangalie tofauti zao zilizopo”, alisema Dogo Janja.

 

Pia, amesema “Kwenye mahusiano kitu pekee kinachozingatiwa ni upendo, kama mnapendana na kuheshimiana vitu vingine ni vya kawaida, binadamu wamekuwa na tabia ya kuhukumu vitu kwa nje lakini hawaujui vizuri undani wake, kwa hiyo ilikuwa moja ya kufikisha ujumbe na burudani pia kwa mashabiki zangu,” alimalizia Janjaro.

CREDIT: EATV

SHORT FILM: MAPENZI YANATESA SANA, USIMCHEKE MTU ANAYELIA KWA SABABU PENZI

Comments are closed.