The House of Favourite Newspapers

Kisa Uchaguzi Simba, Wanachama Watinga Ikulu

 

Wachezaji wa Simba wakiwa na viongozi wa timu.

IMEELEZWA kuwa zaidi ya wanachama 400 wa Klabu ya Simba wamewasilisha barua Ikulu kupinga katiba mpya ya klabu hiyo itakayotumika katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba 3 kwa madai kuwa unawanyima haki ya msingi kwa baadhi ya wanachama ambao hawana shahada.

 

Simba inatarajia kufanya uchaguzi wake, Novemba 3 kuteua mwenyekiti mpya wa klabu hiyo kwa kutumia  katiba mpya iliyopitishwa mwaka 2018 kupitia ibara ya 27, ambapo mwenyekiti lazima awe na shahada aliyosomea katika chuo chochote kinachotambulika

 

serikalini. Uchaguzi huo wa Simba unafanyika katika mfumo wa mabadiliko ambapo wanachama watachagua wajumbe sita akiwemo mwenyekiti ambaye ataongeza wajumbe wengine wawili, na upande wa mwekezaji utakuwa na wajumbe nane. Taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata kutoka Simba, zinasema kuwa wanachama 400 kutoka matawi mbalimbali wakiongozwa na Mzee Hamis Kilomoni wamepeleka barua Ikulu kwa lengo la kupinga katiba hiyo ili haki itendeke kwa wanachama wote.

 

“Katiba mpya ya Simba haipo vizuri, imelenga kuwakandamiza wanachama kwani hata nafasi za wajumbe ambazo zimetajwa hazijaelezwa kazi zao zitakuwa ni zipi mara baada ya kuchaguliwa, pia sehemu ya msemaji katika katiba hiyo haipo, hatuelewi. “Kuna wanachama zaidi ya 400 kutoka matawi mbalimbali wamefika Ikulu kuwasilisha barua yao ya kupinga uchaguzi huo kutokana na katiba inayotumika kutokuwa rafiki kwa wanachama, hivyo wanahitaji Rais John Magufuli aweze kulifanyia kazi suala hilo na walikuwa wakisubiria arejee kutoka katika ziara yake,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Gazeti hili lilimtafuta Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ azungumzie suala hilo lakini simu yake imekuwa ikiita bila ya kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) hakujibu licha ya kuonyesha imefika. Alipotafutwa Mkurugenzi wa Ikulu, Gerson Msigwa kuhusu suala hilo alisema: “Kama wanachama wameandika kwa barua basi watajibiwa kwa barua lakini wanaohusika zaidi ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo watatoa ufafanu

zi kama wameipokea.” Kupitia Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Mkeyenge naye alipotafutwa alisema: “Bado sijaipata barua kama hiyo labda iwe imefika jana (juzi), lakini masuala yote ya soka yapo chini ya TFF ambao ndiyo tunawatumia kufikisha taarifa kwa klabu zao, iwapo kutakuwa na tatizo lolote, Simba wanatakiwa kuanzia huko.”

 

Hadi sasa wadau 21 ndiyo waliochukua fomu kupitia katiba mpya ya 2018 chini ya ibara ya 21 ambao ni Christopher Mwansasu, Dokta Zawadi Ally Kadunda, Abubakar Zebo, Patrick Rweyemamu, Hamisi Mkoma, Ally Suru, Alfred Eliya na Omar Selemani. Wengine ni Mohamed Wandi, Juma Pinto, Said Tully, Mwina Kaduguda, Idd Kajuna, Hussein Mlinga, Jasmeen Badou na Asha Baraka

Comments are closed.