The House of Favourite Newspapers

Kisinda: Bado Hamjaona Kiwango Changu

0

WINGA wa Yanga, Tuisila Kisinda amesema kuwa anajiona bado hajacheza katika kiwango chake cha juu, lakini atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anatoa mchango mkubwa kwa timu.

 

Yanga katika mchezo unaofuta wa ligi wanatarajiwa kumenyana na Mtibwa Sugar keshokutwa Jumapili katika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.Kisinda amejiunga na Yanga akitokea katika klabu ya AS Vita ya DRC Congo ambapo tangu ajiunge na timu hiyo amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, winga huyo amesema kuwa bado hajacheza na kufikia katika kiwango chake cha juu lakini atajitahidi kuhakikisha anaisaidia Yanga kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya ligi kuu.

“Mashabiki wanatakiwa kuwa na subira lakini waendelee kuiunga mkono timu yao, kwa upande wangu bado sijacheza katika kiwango kizuri lakini naamini huko mbeleni kwenye michezo ijayo nitafanya mambo makubwa.

 

“Kuhusu Ligi ya Tanzania kuna mambo najifunza kupitia ligi hii ambayo nimegundua kuwa ina wachezaji wengi wazuri na ina ushindani mkubwa hivyo inahitaji kupambana ili kupata matokeo na mimi nipo tayari kwa hilo,” alisema Kisinda.Kisinda katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Kagera Sugar alifanikiwa kutoa pasi ya bao liliofungwa na Tonombe Mukoko katika ushindi wa bao 1-0.

Leave A Reply