The House of Favourite Newspapers

Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), UNDP na Wizara ya Uwekezaji Waandaa Kongamano

0
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini, Bwana John Mnali akizungunza kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani)  jijini Dar es Salaam leo.

 

28 Novemba 2022: KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Taifa linaloshughulikia maendeleo la UNDP na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kwa pamoja wameandaa kongamano maalum la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kwa sekta kipaumbele zenye mlengo wa maendeleo endelevu Tanzania.

Mkutano huo ukiendelea.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo Mkurugenzi Kituo cha Uwekezaji nchini, John Mnali amesema kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Rotana hapa jijini Dar-es-salaam na baadaye kutembelea miradi siku ya tarehe 01 Desemba 2022.

 

Mkurugenzi huyo amesema mgeni rasmi katika kongamano anatarajia kuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Akielezea lengo la kongamano hilo Mkurugenzi huyo amesema ni kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zenye mlengo wa maendeleo endelevu zilizopo hapa nchini kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa kutoka nchi mbalimbali duniani.

“Fursa ambazo zipo katika sekta za kipaumbele zenye mlengo wa maendeleo endelevu ni pamoja na sekta ya Kilimo na chakula, Miundombinu, Nishati, Elimu, huduma na nk”. Alimaliza kusema Mkurugenzi huyo.

Leave A Reply