The House of Favourite Newspapers

Kiungo Fundi Ashusha Presha Simba, Ahmed Ally Afunguka

0

 

KUREJEA kwa kiungo fundi raia wa DR Congo, Fabrice Ngoma kumeipa matumiani makubwa timu hiyo, katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara ukiwemo dhidi ya Azam FC.

Kiungo huyo aliukosa mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa FC sambamba na ule wa jana mbele ya Tabora United kutokana na kuwepo nyumbani kwao DR Congo.

Mkongomani huyo anaunda safu ya kiungo ukabaji inayochezwa na Babacar Sarr, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa kiungo huyo juzi Jumatatu alianza mazoezi mepesi akitokea kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia baada ya uongozi kutoa baraka za kwenda huko.

Ahmed alisema kuwa kiungo huyo alianza kwa mazoezi mepesi kuhakikisha anakuwa fiti na tayari kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi ukiwemo dhidi ya Azam FC watakaoucheza Ijumaa ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Aliongeza kuwa kurejea kwa Ngoma kutaimarisha safu yao ya kiungo katika kujiandaa mchezo dhidi ya Azam, ambao anaamini ni mgumu kwao kutokana na upinzani unaokuwepo wanapokutana.

“Jana (juzi) jioni Ngoma alianza mazoezi mepesi ya binafsi hapa Tabora kujiandaa na michezo ijayo ya ligi na kimataifa, baada ya kurejea nchini akitokea kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia.

“Ngoma alikosekana katika michezo miwili, lakini katika michezo ijayo ya ligi, anatarajiwa kuwepo kuipambania timu yake ukiwemo huu wa Dabi ya Mzizima dhidi ya Azam.

“Uwepo wake katika mchezo huu dhidi ya Azam, ataimarisha safu ya kiungo ukabaji, akisaidiana na wenzake akina Sarr, Kanoute, Mzamiru na wengine kuhakikisha tunaimilika safu ya kiungo,” alisema Ahmed.

STORI NA WILBERT MOLANDI

#EXCLUSIVE: MR ROMANTIC wa CHEKA TU – ”NAPENDA WANAWAKE WATAALAM”…

Leave A Reply